<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><lyrics>[V1]
 Roho yangu hima, na taa yako
 Kaiwashe vyema, hapa si pako;
 Nguvu zote pia za duniani
 Hazitakudhuru ukiamini.

[V2]
 Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma,
 Yesu vivyo kando, walindwa vyema.

[V3]
 Adui shetani, na nguvu zake,
 Bwana ameshinda, kwa kifo chake;
 Wewe nguvu huna, huna kabisa,
 Ndiwe mpungufu, mnyonge hasa.

[V4]
 Toka na mapema, mbele ya wote,
 Omba, bisha sana, maisha yote;
 Vita vikaliko, macho ukae,
 Jivike silaha, nawe sishindwe.

[V5]
 Bwana Yesu ndiye kwako mchunga,
 Neno lake Bwana ndilo upanga;
 Mbingu zitakwisha, na nchi pia,
 Neno lake Bwana laendelea.</lyrics>
<title>Roho Yangu Hima TZR21</title>
<hymn_number>21</hymn_number>
</song>